Tuesday, 20 May 2025
MKATABA WA KUKODISHA NYUMBA
Wednesday, 17 August 2022
MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA
MKATABA
WA KUPANGISHA NYUMBA
KATI
YA
…….………………………………………………….
(MWENYE
NYUMBA)
NA
………………………………………………………….
MPANGAJI
KATIKA
NYUMBA ILIYOPO
………………………………………………………
MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA.
MKATABA huu umefanyika leo tarahe ……….… mwezi wa ………….., mwaka ………………… kati ya Bwana
………………………………………wa Sanduku la Posta ………………………………………., kwa upande mmoja (ambaye
katika mkataba huu ataitwa “MWENYE NYUMBA”), NA …………………………………………..… wa Sanduku
la Posta ………………….. , …………………………. (ambaye katika mkataba huu ataitwa “MPANGAJI”.
KWA KUWA mwenye nyumba ni mmiliki halali wa nyumba yenye vyumba ………………………… vya kulala, sebule, choo na bafu, jiko, chumba cha kulia chakula iliyopo kwenye kitalu namba …………………………………, katika Manispaa ya .................... mkoani ....................
na
KWA KUWA mpangaji amemwendea mwenye nyumba kwa nia
ya kutaka kupangisha nyumba hiyo kwa muda wa kipindi cha mwaka mmoja kwa malipo
ya kodi iliyokubaliwa katika mkataba huu na kwa mujibu wa masharti mengineyo
yatakayoafikiwa kwenye mkataba huu; na
KWA KUWA mwenye nyumba mwenye nyumba amekubali
kumpangisha mpangaji katika nyumba hiyo;
HIVYO
BASI, MKATABA huu unashuhudia na kuthibitisha
1. KWAMBA
Mwenye nyumba amempangisha mpangaji nyumba hiyo iliyopo katika eneo lililotajwa
hapo juu kwa kiasi cha kodi ya Tshs. ………………………………….. tu, (Tshs. ……………………….) kwa
mwezi na kwamba fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo kwa kwa kipindi chote cha ………………………………
cha mkataba huo yaani jumla ya Tshs. ………………………………tu (Tshs. …………………………).
2. KWAMBA
mpangaji ataanza kupanga nyumba hiyo kuanzia tarehe ……….. mwezi ………………. Mwaka …………………………….
ambapo mkataba huo utakoma.
3. KWAMBA,
ikiwa Mpangaji anatimiza masharti yote ya ulipaji kodi na mengineyo, Mwenye
nyumba anampangisha mpangaji nyumba hiyo bila kumuingilia katika kipindi chote
cha upangaji huo.
4. KWAMBA
Mpangaji anatakiwa azingatie usafi wa nyumba pamoja na mazingira yake na
anatakiwa atumie nyumba hiyo kwa matumizi ya makazi tu na sio vinginevyo na
yote haya yanafanyika pasipo kufanya shughuli nyingine yoyote katika nyumba
hiyo ambacho kitakuwa ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
5. KWAMBA
Mpangaji anatakiwa azingatie kulipa kodi kama inavyotakiwa na kuilipa kwa
wakati
6. KWAMBA
Mwenye nyumba, kwa wakati muafaka anayo haki ya kuingia katika nyumba hiyo pale
inapobidi ili kukagua au kufanya ukarabati wa nyumba hiyo.
7. KWAMBA
Mpangaji anatakiwa aiweke nyumba hiyo anayopanga katika hali ya usafi wakati
wote na kuhakikisha kwamba kuta na sehemu zingine za chumba haziharibiwi.
8. KWAMBA
Mpangaji anatakiwa alipie maji, umeme au simu katika nyumba hiyo kwa muda wote
atakaopanga nyumnba hiyo na wakati wa kuondoka katika nyumba hii atahakikisha
kuwa hataacha madeni yoyote yanayohusiana na umeme, maji au simu.
9. KWAMBA
Mpangaji haruhusiwi kufanya matengenezo au marekebisho yoyote katika nyumba
hiyo aliyopanga bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwenye nyumba kwa muda
watakaokubaliana.
10. KWAMBA
Mpangaji haruhisiwi kukodisha nyumba hiyo aliyopanga kwa mtu mwingine yeyote
bila ya idhini ya maandishi kutoka kwa Mwenye Nyumba, na ikiwa Mpangaji atashindwa
kuendelea na Mkataba basi mpangaji atamrudishia nyumba mwenye nyumba.
11. KWAMBA
Mpangaji ahakikishe kwamba kwa wakati wote atakaokuwa kwenye nyumba hiyo hatawaghasi
majirani wenzake kwa njia yoyote ile.
12.
KWAMBA Mpangaji amjulishe mwenye nyumba kwa maandishi mwanzo wa mwezi mmoja (1)
wa mwisho wa mkataba huu endapo atapenda kuendelea na mkataba huu mara
utakapokwisha.
13.
KWAMBA Mpangaji na Mwenye nyumba wanaweza kusitisha mkataba huu kwa kutoa
taarifa kwa maandishi mwezi mmoja kabla.
14. KWAMBA
Maneno “Mwenye Nyumba” na “Mpangaji” yatahusu familia, jamii na wategemea wa
kila mmoja wao kwa madhumuni ya mkataba huu.
KWA USHUHUDA na UTHIBITISHO, mkataba huu umewekwa
sahihi na Mwenye Nyumba na Mpangaji mbele ya mashahidi
IMETIWA
SAHIHI na KUTOLEWA )
na …………………………..
leo hii ) ...................................
tarehe
….. mwezi ……….. mwaka ………. ) MWENYE NYUMBA
Mbele
ya:-
Jina: ……………………………………
Wadhifa: ……………………………………
Sahihi:-
……………………………………………
Tarehe: ……………………………………
IMETIWA
SAHIHI na KUTOLEWA )
na ………………………………….
leo hii ) ..................................
tarehe
….. mwezi ……….. mwaka ……….. ) MWENYE NYUMBA
Mbele
ya:-
Jina: ……………………………………
Wadhifa: ……………………………………
Sahihi:-
……………………………………………
Tarehe: ……………………………………
Umeandaliwa na:-
…………………………………..
S.
L. Posta