Showing posts with label mkataba. Show all posts
Showing posts with label mkataba. Show all posts

Wednesday, 21 May 2025

Uhumuhimu wa Kuwa na Mkataba Wa Maandishi wa Kukodisha Nyumba

Uhumuhimu wa Kuwa na Mkataba Wa Maandishi wa Kukodisha Nyumba

Kukodisha au kukodi nyumba ni moja kati ya mikataba muhimu katika maisha ya kila siku. Hata hivyo, wakati mwingine watu hufanya makubaliano kwa maneno pekee (verbal agreement) na baadaye kukumbana na migogoro. Ndio maana kuwa na mkataba wa maandishi wa kukodisha nyumba ni muhimu kwa mkodishaji (landlord) na mkodi (tenant). Hapa kuna sababu kuu:

1. Kuepuka Migogoro na Kutoelewana

Mkataba wa maandishi unaweka wazi masharti yote kama vile:

Kodi ya kila mwezi

Amana (deposit) na masharti ya kurudishwa

Majukumu ya kila mtu (matengenezo, malipo, n.k)

Bila mkataba, mtu anaweza kugeuka mwenendo au kukanusha makubaliano, na kusababisha mzozo.


2. Kulinda Haki za Pande Zote

Mkataba wa maandishi ni uthibitisho wa kisheria unaoweza kutumika mahakamani ikiwa kutakuwa na malalamiko. Kwa mfano:

Mkodi anaweza kudai kurudishiwa amana yake kwa mujibu wa mkataba.

Mkodishaji anaweza kumfukuza mkodi kwa ukiukwaji wa masharti.


3. Kuepuka Udanganyifu na Uvivu wa Malipo

Baadhi ya wakodishaji au wakodi wanaweza kujifanya kusahau au kubadilisha mikataba kiholela. Mkataba waandishi:

Huweka tarehe kamili za malipo na faini za ucheleweshaji.

Huruhusu mwenye nyumba kuchukua hatua za kisheria ikiwa mkodi hatolipi kwa muda mrefu.


4. Kufuata Sheria na Udhibiti wa Makubaliano

Nchi nyingi zina sheria maalum za ukodishaji zinazohitaji mkataba rasmi. Kwa kuwa na hati sahihi:

Unakwepa matatizo na vikwazo vya kisheria.

Unathibitisha kuwa mkataba wako unaweza kutumika kama ushahidi ikiwa kutahitajika.


5. Kuwa na Rejea ya Kumbukumbu

Mkataba waandishi ni kama rejea ya kudumu ambayo inaweza kukumbusha pande zote kuhusu:

Muda wa mkataba (miezi/miaka)

Vipengee vilivyokubaliwa (kama vile marupurupu ya matengenezo)

Hitimisho

Kukodisha nyumba bila mkataba waandishi ni sawa na kutembea kwenye barabara bila bima – unaweza kufika salama, lakini ikiwa kuna shida, unaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa. Kwa hivyo, hakikisha unatengeneza mkataba wazi na sahihi kabla ya kukodisha au kukodi nyumba yoyote.

Je, una mkataba wa kukodisha nyumba? Kama hauna, ni wakati muafaka wa kuandaa moja!

(Makala hii inakuletea ufahamu wa muhimu ya mikataba ya kukodisha. Kama unahitaji msaada wa kuandaa mkataba, tafadhali wasiliana na mwanasheria

Wednesday, 17 August 2022

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA

 

 Below is a swahili contract for leasing a house.

 

 

 

 

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA

 

 

 

KATI YA

 

 

 

 

…….………………………………………………….

(MWENYE NYUMBA)

 

 

 

 

NA

 

 

 

 

 

………………………………………………………….

MPANGAJI

 

 

 

 

 

KATIKA NYUMBA ILIYOPO

 

………………………………………………………

 

 

 

 

 

 

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA.

 

MKATABA huu umefanyika leo tarahe  ……….… mwezi wa ………….., mwaka ………………… kati ya Bwana ………………………………………wa Sanduku la Posta ………………………………………., kwa upande mmoja (ambaye katika mkataba huu ataitwa “MWENYE NYUMBA”), NA …………………………………………..… wa Sanduku la Posta ………………….. , …………………………. (ambaye katika mkataba huu ataitwa “MPANGAJI”.

 

KWA KUWA mwenye nyumba ni mmiliki halali wa nyumba yenye vyumba ………………………… vya kulala, sebule, choo na bafu, jiko, chumba cha kulia chakula iliyopo kwenye kitalu namba …………………………………, katika Manispaa ya .................... mkoani ....................

 na

 

KWA KUWA mpangaji amemwendea mwenye nyumba kwa nia ya kutaka kupangisha nyumba hiyo kwa muda wa kipindi cha mwaka mmoja kwa malipo ya kodi iliyokubaliwa katika mkataba huu na kwa mujibu wa masharti mengineyo yatakayoafikiwa kwenye mkataba huu; na

 

KWA KUWA mwenye nyumba mwenye nyumba amekubali kumpangisha mpangaji katika nyumba hiyo;

 

 

HIVYO BASI, MKATABA huu unashuhudia na kuthibitisha kama ifuatavyo:

 

1.        KWAMBA Mwenye nyumba amempangisha mpangaji nyumba hiyo iliyopo katika eneo lililotajwa hapo juu kwa kiasi cha kodi ya Tshs. ………………………………….. tu, (Tshs. ……………………….) kwa mwezi na kwamba fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo kwa kwa kipindi chote cha ……………………………… cha mkataba huo yaani jumla ya Tshs. ………………………………tu (Tshs. …………………………).

 

2.        KWAMBA mpangaji ataanza kupanga nyumba hiyo kuanzia tarehe ……….. mwezi ………………. Mwaka ……………………………. ambapo mkataba huo utakoma.

 

3.        KWAMBA, ikiwa Mpangaji anatimiza masharti yote ya ulipaji kodi na mengineyo, Mwenye nyumba anampangisha mpangaji nyumba hiyo bila kumuingilia katika kipindi chote cha upangaji huo.

 

4.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa azingatie usafi wa nyumba pamoja na mazingira yake na anatakiwa atumie nyumba hiyo kwa matumizi ya makazi tu na sio vinginevyo na yote haya yanafanyika pasipo kufanya shughuli nyingine yoyote katika nyumba hiyo ambacho kitakuwa ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

 

5.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa azingatie kulipa kodi kama inavyotakiwa na kuilipa kwa wakati kama ilivyokubaliwa katika mkataba huu.

  

6.        KWAMBA Mwenye nyumba, kwa wakati muafaka anayo haki ya kuingia katika nyumba hiyo pale inapobidi ili kukagua au kufanya ukarabati wa nyumba hiyo.

 

7.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa aiweke nyumba hiyo anayopanga katika hali ya usafi wakati wote na kuhakikisha kwamba kuta na sehemu zingine za chumba haziharibiwi.

 

8.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa alipie maji, umeme au simu katika nyumba hiyo kwa muda wote atakaopanga nyumnba hiyo na wakati wa kuondoka katika nyumba hii atahakikisha kuwa hataacha madeni yoyote yanayohusiana na umeme, maji au simu.

 

9.        KWAMBA Mpangaji haruhusiwi kufanya matengenezo au marekebisho yoyote katika nyumba hiyo aliyopanga bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwenye nyumba kwa muda watakaokubaliana.

 

10.      KWAMBA Mpangaji haruhisiwi kukodisha nyumba hiyo aliyopanga kwa mtu mwingine yeyote bila ya idhini ya maandishi kutoka kwa Mwenye Nyumba, na ikiwa Mpangaji atashindwa kuendelea na Mkataba basi mpangaji atamrudishia nyumba mwenye nyumba.

 

11.      KWAMBA Mpangaji ahakikishe kwamba kwa wakati wote atakaokuwa kwenye nyumba hiyo hatawaghasi majirani wenzake kwa njia yoyote ile.

 

12.      KWAMBA Mpangaji amjulishe mwenye nyumba kwa maandishi mwanzo wa mwezi mmoja (1) wa mwisho wa mkataba huu endapo atapenda kuendelea na mkataba huu mara utakapokwisha.

 

13.      KWAMBA Mpangaji na Mwenye nyumba wanaweza kusitisha mkataba huu kwa kutoa taarifa kwa maandishi mwezi mmoja kabla.   

 

14.      KWAMBA Maneno “Mwenye Nyumba” na “Mpangaji” yatahusu familia, jamii na wategemea wa kila mmoja wao kwa madhumuni ya mkataba huu.

 

KWA USHUHUDA na UTHIBITISHO, mkataba huu umewekwa sahihi na Mwenye Nyumba na Mpangaji mbele ya mashahidi kama inavyoonyeshwa hapa chini:

 

 

 

IMETIWA SAHIHI na KUTOLEWA                     )

na ………………………….. leo hii                     )    ...................................

tarehe ….. mwezi ……….. mwaka ……….      )    MWENYE NYUMBA

 

Mbele ya:-

 

Jina:               ……………………………………

 

Wadhifa:       ……………………………………

 

Sahihi:- ……………………………………………

 

Tarehe:         ……………………………………

 

 

 

IMETIWA SAHIHI na KUTOLEWA                     )

na …………………………………. leo hii             )           ..................................

tarehe ….. mwezi ……….. mwaka ………..     )           MWENYE NYUMBA

 

Mbele ya:-

 

Jina:               ……………………………………

 

Wadhifa:       ……………………………………

 

Sahihi:- ……………………………………………

 

Tarehe:         ……………………………………

 

 

 

Umeandaliwa na:-

 

…………………………………..

S. L. Posta

Dar es Salaam