Showing posts with label mkataba waupangishaji nyumba. Show all posts
Showing posts with label mkataba waupangishaji nyumba. Show all posts

Wednesday, 17 August 2022

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA

 

 Below is a swahili contract for leasing a house.

 

 

 

 

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA

 

 

 

KATI YA

 

 

 

 

…….………………………………………………….

(MWENYE NYUMBA)

 

 

 

 

NA

 

 

 

 

 

………………………………………………………….

MPANGAJI

 

 

 

 

 

KATIKA NYUMBA ILIYOPO

 

………………………………………………………

 

 

 

 

 

 

MKATABA WA KUPANGISHA NYUMBA.

 

MKATABA huu umefanyika leo tarahe  ……….… mwezi wa ………….., mwaka ………………… kati ya Bwana ………………………………………wa Sanduku la Posta ………………………………………., kwa upande mmoja (ambaye katika mkataba huu ataitwa “MWENYE NYUMBA”), NA …………………………………………..… wa Sanduku la Posta ………………….. , …………………………. (ambaye katika mkataba huu ataitwa “MPANGAJI”.

 

KWA KUWA mwenye nyumba ni mmiliki halali wa nyumba yenye vyumba ………………………… vya kulala, sebule, choo na bafu, jiko, chumba cha kulia chakula iliyopo kwenye kitalu namba …………………………………, katika Manispaa ya .................... mkoani ....................

 na

 

KWA KUWA mpangaji amemwendea mwenye nyumba kwa nia ya kutaka kupangisha nyumba hiyo kwa muda wa kipindi cha mwaka mmoja kwa malipo ya kodi iliyokubaliwa katika mkataba huu na kwa mujibu wa masharti mengineyo yatakayoafikiwa kwenye mkataba huu; na

 

KWA KUWA mwenye nyumba mwenye nyumba amekubali kumpangisha mpangaji katika nyumba hiyo;

 

 

HIVYO BASI, MKATABA huu unashuhudia na kuthibitisha kama ifuatavyo:

 

1.        KWAMBA Mwenye nyumba amempangisha mpangaji nyumba hiyo iliyopo katika eneo lililotajwa hapo juu kwa kiasi cha kodi ya Tshs. ………………………………….. tu, (Tshs. ……………………….) kwa mwezi na kwamba fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo kwa kwa kipindi chote cha ……………………………… cha mkataba huo yaani jumla ya Tshs. ………………………………tu (Tshs. …………………………).

 

2.        KWAMBA mpangaji ataanza kupanga nyumba hiyo kuanzia tarehe ……….. mwezi ………………. Mwaka ……………………………. ambapo mkataba huo utakoma.

 

3.        KWAMBA, ikiwa Mpangaji anatimiza masharti yote ya ulipaji kodi na mengineyo, Mwenye nyumba anampangisha mpangaji nyumba hiyo bila kumuingilia katika kipindi chote cha upangaji huo.

 

4.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa azingatie usafi wa nyumba pamoja na mazingira yake na anatakiwa atumie nyumba hiyo kwa matumizi ya makazi tu na sio vinginevyo na yote haya yanafanyika pasipo kufanya shughuli nyingine yoyote katika nyumba hiyo ambacho kitakuwa ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

 

5.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa azingatie kulipa kodi kama inavyotakiwa na kuilipa kwa wakati kama ilivyokubaliwa katika mkataba huu.

  

6.        KWAMBA Mwenye nyumba, kwa wakati muafaka anayo haki ya kuingia katika nyumba hiyo pale inapobidi ili kukagua au kufanya ukarabati wa nyumba hiyo.

 

7.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa aiweke nyumba hiyo anayopanga katika hali ya usafi wakati wote na kuhakikisha kwamba kuta na sehemu zingine za chumba haziharibiwi.

 

8.        KWAMBA Mpangaji anatakiwa alipie maji, umeme au simu katika nyumba hiyo kwa muda wote atakaopanga nyumnba hiyo na wakati wa kuondoka katika nyumba hii atahakikisha kuwa hataacha madeni yoyote yanayohusiana na umeme, maji au simu.

 

9.        KWAMBA Mpangaji haruhusiwi kufanya matengenezo au marekebisho yoyote katika nyumba hiyo aliyopanga bila idhini ya maandishi kutoka kwa mwenye nyumba kwa muda watakaokubaliana.

 

10.      KWAMBA Mpangaji haruhisiwi kukodisha nyumba hiyo aliyopanga kwa mtu mwingine yeyote bila ya idhini ya maandishi kutoka kwa Mwenye Nyumba, na ikiwa Mpangaji atashindwa kuendelea na Mkataba basi mpangaji atamrudishia nyumba mwenye nyumba.

 

11.      KWAMBA Mpangaji ahakikishe kwamba kwa wakati wote atakaokuwa kwenye nyumba hiyo hatawaghasi majirani wenzake kwa njia yoyote ile.

 

12.      KWAMBA Mpangaji amjulishe mwenye nyumba kwa maandishi mwanzo wa mwezi mmoja (1) wa mwisho wa mkataba huu endapo atapenda kuendelea na mkataba huu mara utakapokwisha.

 

13.      KWAMBA Mpangaji na Mwenye nyumba wanaweza kusitisha mkataba huu kwa kutoa taarifa kwa maandishi mwezi mmoja kabla.   

 

14.      KWAMBA Maneno “Mwenye Nyumba” na “Mpangaji” yatahusu familia, jamii na wategemea wa kila mmoja wao kwa madhumuni ya mkataba huu.

 

KWA USHUHUDA na UTHIBITISHO, mkataba huu umewekwa sahihi na Mwenye Nyumba na Mpangaji mbele ya mashahidi kama inavyoonyeshwa hapa chini:

 

 

 

IMETIWA SAHIHI na KUTOLEWA                     )

na ………………………….. leo hii                     )    ...................................

tarehe ….. mwezi ……….. mwaka ……….      )    MWENYE NYUMBA

 

Mbele ya:-

 

Jina:               ……………………………………

 

Wadhifa:       ……………………………………

 

Sahihi:- ……………………………………………

 

Tarehe:         ……………………………………

 

 

 

IMETIWA SAHIHI na KUTOLEWA                     )

na …………………………………. leo hii             )           ..................................

tarehe ….. mwezi ……….. mwaka ………..     )           MWENYE NYUMBA

 

Mbele ya:-

 

Jina:               ……………………………………

 

Wadhifa:       ……………………………………

 

Sahihi:- ……………………………………………

 

Tarehe:         ……………………………………

 

 

 

Umeandaliwa na:-

 

…………………………………..

S. L. Posta

Dar es Salaam