Showing posts with label sheria. Show all posts
Showing posts with label sheria. Show all posts

Friday, 26 August 2022

MAOMBI YA FARAGHA YA KUONGEZEWA MUDA

 KATIKA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

KATIKA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA ILALA

LILILOPO JENGO LA MWALIMU

MAOMBI MADOGO NAMBA ____ YA MWAKA 2022

(Yanayotokana na maombi namba ......... ya mwaka 2022)

BAINA YA

XXX.............................................. MLETA MAOMBI

DHIDI

YYY ..............................MJIBU MAOMBI


MAOMBI YA FARAGHA

(Yanafanywa chini ya kifungu cha 14 cha sheria ya Ukomo wa muda sura ya 89 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019, na sheria nyingine yoyote itakayohusika)


PANDE ZOTE WANAOHUSIKA WAFIIKE, mbele ya Mheshimiwa..................Mwenyekiti wa Baraza katika chumba cha Mwenyekiti tarehe ......... mwezi wa ...... mwaka 2022, au katika muda utakaoamriwa, ambapo mwombaji atasikilizwa maombi yake kwa kupatiwa amri zifuatazo: -

1. Kwamba mahakama itoe ruhusa kwa mleta maombi kuongezewa muda ili afanye maombi ya kutengua hukumu ya upande mmoja iliyotolewa katika maombi namba....... la mwaka 2022.

2. Mahakama itoe nafuu nyingine yoyote kwa kwa kadiri itakavyo ona ni haki kutoa.

Maombi haya yanafanywa na  kwa sambamba sababu vigezo na sababu zilivotajwa katika kiapo cha mleta maombi XXX ambacho kimeambatanishwa katika maombi haya na sababu za ziada zitatolewa na mleta maombi wakati wa kusikilizwa maombi haya.

...........................................

MWENYEKITI


Yameletwa kusajilwa leo hii ...................... Siku ya mwezi wa ...................mwaka 2022.

...........................................

KARANI WA BARAZA


YAMEANDALIWA NA

XXX, MLETA MAOMBI,

S.L.P.

DAR ES SALAAM,

TANZANIA


NAKALA APATIWE

YYY, MJIBU MAOMBI

Wednesday, 24 August 2022

Je, Unaweza kufungwa kama mfungwa wa kesi ya madai?

 Je unaweza kufungwa kama mfungwa wa kesi ya madai? 

Jibu fupi ni NDIYO. 

Kukamatwa na kuwekwa kizuizini kama mfungwa wa kesi ya madai bado ni mojawapo ya njia ambazo hukumu ya mahakama inaweza kutekelezwa nchini Tanzania.

Kifungu cha 44 kikisomwa pamoja na Order namba XXI Kanuni ya 10(2)(j)(iii) na Kanuni ya 35 ya kanuni ya mwenendo wa kesi za madai zinatambua kukamatwa na kufungwa kama mojawapo ya njia ambazo amri ya mahakama inaweza kutekelezwa.

Kesi za kusoma: 

  1. Harel Mallac Tanzania Limited V Junaco (T) Limited and Another, Miscellaneous Commercial Application No. 144 Of 2016, High Court (Commercial Division), (Unreported)
  2. Omari Mzee Mtumweni v Said Issa Magenza, Civil Case No. 88 of 1987 , High Court Dar Es Salaam, (Unreported)
  3. Harel Mallac Tanzania Limited V Junaco (T) Limited, Miscellaneous Commercial Application No. 144 of 2016, High Court (Commercial Division), (Unreported).
  4. THE GRAND ALLIANCE LIMITED versus MR. WILFRED LUCAS TARIMO and others. CIVIL APPLICATION NO. 187/16 OF 2019
  5. ESTHER CRESCENCE MASHOKO versus NORBERT FURAHA LYIMO MISC. LAND CASE APPLICATION NO. 90 OF 2016
  6. JOSEPH NESTORY ISAKA versus FLANCONIA INVESTMENT LTD EXECUTION NO. 4 OF 2020 (From Execution Land Case No.118 of 2015)