Wednesday, 17 August 2022

Mkataba wa mauziano ya eneo

MKATABA WA MAUZIANO YA SHAMBA

 

MAKUBALIANO HAYA YAMEFANYIKA siku ya tarehe _____ mwezi __________, Mwaka 2022

BAINA YA:

ndugu________________________ (mwenye kitambulisho cha taifa namba ___________________________)  wa sanduku la posta ___________ _______

na

ndugu ________________________ (mwenye kitambulisho cha taifa namba ___________________________), wa sanduku la posta ________ _______ambaye ndani ya mkataba huu watakua wanatajwa kama WAUZAJI; KWA UPANDE MMOJA

NA

Ndugu ___________________________ wa sanduku la posta _______, Dar es Salaam, ambaye ndani ya mkataba huu atakua anatajwa kama MNUNUZI. KWA UPANDE WA PILI

KWA KUWA:

a. WAUZAJI ndiye wamiliki halali wa eneo eneo linalouzwa lenye ukubwa wa __________________ ambalo lipo katika eneo la ____________, Kitongoji cha ________________________, Kata ya ________________________, Wilaya Ya ________________________, mkoa wa _______________________

b.   MNUNUZI kwa hiari yake mwenyewe ameridhia na ameamua kununua nyumba kama ilivyotajwa na Mkataba huu, na hasa baada ya kuikagua na kuridhika

WAHUSIKA WA MKATABA HUU WANAKUBALIANA YAFUATAYO:

1.      KWAMBA Wauzaji ni wamiliki halali wa eneo linalouzwa lenye ukubwa wa __________________ ambalo lipo katika eneo la ____________, Kitongoji cha ________________________, Kata ya ________________________, Wilaya Ya ________________________, mkoa wa ________________________na ambalo limetambuliwa na kuonyeshwa kwa Mnunuzi na mipaka yake yote mbele ya mashahidi waliotajwa na kuweka sahihi zao katika hati hii kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

2.      KWAMBA Wauzaji wakiwa na akili timamu na kwa hiari zao wanamuuzia Mnunuzi eneo hilo lenye ukubwa wa ekari tano bei ya TZS__________________ (Shilingi ya Kitanzania __________________Tu)

3.      KWAMBA Wauzaji wanauza eneo hilo likiwa halina migogoro yoyote na haliko chini ya madai yoyote na kwamba umiliki wa Muuzaji wa shamba hilo haugombaniwi wala kubishaniwa na mtu yoyote.

4.      KWAMBA endapo Mnunuzi atapoteza umiliki wa shamba hilo kutokana na Muuzaji kutokuwa na umiliki halali na dhabiti au eneo hilo kuwa na mgogoro au migogoro ya umiliki imhusishayo au kumhusu Muuzaji kwa jinsi yoyote ile, basi Wauzaji watalazimika kumlipa Mnunuzi pesa zake zote alizomlipa kununua eneo hilo pamoja na riba na gharama ambazo Mnunuzi atakuwa ameingia kutokana na mgogoro au migogoro hiyo.

5.      KWAMBA Mnunuzi leo hii tarehe ya mkataba huu amewalipa wauzaji jumla ya TZS__________________ (Shilingi ya Kitanzania __________________Tu) ikiwa ni bei kamili ya mauzo ya eneo hilo na Wauzaji kwa mkataba huu wanakiri kupokea fedha hizo zote na hawana madai yoyote dhidi ya Mnunuzi.

6.      KWAMBA kwa mkataba huu Wauzaji wanamkabidhi Mnunuzi eneo hilo liwe katika milki yake moja kwa moja na hawataingilia umiliki wa Mnunuzi.

7.     KWAMBA maneno “Wauzaji” na “Mnunuzi” yatahusu familia, jamii na wategemea wa kila mmoja wao kwa madhumuni ya mkataba huu.

8.      KWAMBA migogoro yoyote itakayotokana na tafsiri ya Mkataba huu, au jambo jingine lolote litokanalo na Mkataba  huu au mauzo yaliyofanyika, litatatuliwa na pande mbili husika kwa namna itakavyopendekezwa na wahusika wenyewe,  isipokuwa pale utatuzi unaposhindikana, basi mgogoro au jambo hilo litatatuliwa na vyombo vinavyofahamika kisheria, kwa kutumia Sheria za Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania.

 NA INASHUHUDIWA kwamba wahusika katika mkataba huu wameingia mkataba huu siku hii kama inavyo onekana hapo chini:


Mkataba UMESAINIWA na

________________________, siku hii                                                          

ya tarehe ______mwezi wa_____________2022                         Saini ya Muuzaji

 


Mkataba UMESAINIWA na

________________________, siku hii                                                                                                                 

ya tarehe ______mwezi wa_____________2022                          Saini ya Muuzaji

                                                                                           

MBELE YA MASHAIDI

JINA LA SHAHIDI: ________________________

Sahihi: ___________________________                                                                        

Wadhifa: ________________________ 

Anuani: ______________________

Tarehe: _______________________

 

JINA LA SHAHIDI: ________________________

Sahihi: _________________________

Wadhifa:________________________

Anuani: ________________________

Tarehe: _________________________



Mkataba UMESAINIWA na

________________________________

ambaye ninamfahamu katika siku hii ya                             ____________________

tarehe 18 mwezi wa nane, 2022                                           Saini ya Muuzaji

 

MBELE YANGU

Sahihi:_________________________                              

Jina ___________________________                             

Anuani:________________________

Wadhifa _______________________

 


No comments:

Post a Comment